Equity yatangaza matokeo ya kifedha 2025, yapata faida 55%

DAR ES SALAAM: Equity Bank Group Holdings Plc imetangaza matokeo yake ya mwaka mzima ya mwaka 2025, yakiwa ni ya kihistoria na yenye kuashiria mafanikio makubwa baada ya faida yake baada ya kodi kuongezeka kwa asilimia 55 na kufikia Kshs bilioni 75.5.

Ukuaji huu wa rekodi unathibitisha mafanikio ya mkakati wa mageuzi ya kampuni hii, unaochochewa na vyanzo mbalimbali vya mapato, kuboreshwa kwa ufanisi wa utendaji kazi, pamoja na mchango mkubwa kutoka matawi yake ya kila nchi.

Mizania ya kikundi imeongezeka na kufikia Kshs trilioni 1.97, ikiungwa mkono na ukuaji mkubwa wa amana za wateja na mfumo imara wa kidijitali ambao sasa unahudumia zaidi ya asilimia 88 ya miamala yote.

Benki ya Equity Bank Tanzania imeonesha kiwango cha juu cha utendaji, chini ya uongozi wa Mkurugenzi Mkuu wake Bi. Isabela Maganga, ambapo tawi hili la Tanzania limepata ukuaji wa kushangaza wa asilimia 125 katika faida yake baada ya kodi, na kufikia Kshs bilioni 2.7.

Matokeo haya bora yameungwa mkono na ukuaji wa asilimia 75 katika mtaji wa wanahisa, ikionesha nguvu ya mtaji na uthabiti wa mizania pamoja na upanuzi wa asilimia 61 ya mikopo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Group Dr.James Mwangi ameeleza kuwa mafanikio haya makubwa yanatokana na mkakati wa benki wa kuzingatia ubunifu na mageuzi yake zaidi ya shughuli za kibenki za kawaida.

Alisisitiza kuwa benki inaendeleza kuwa taasisi iliyo tayari kwa mustakabali kwa kutumia uwezo wa kisasa wa kidijitali na ule unaotegemea Akili Bandia (AI) ili kuboresha uzoefu wa wateja na kupunguza gharama za utoaji huduma.

“Lengo letu ni kujenga taasisi iliyo tayari kwa mustakabali, yenye uwezo wa kukua, yenye usalama na inayoongozwa na athari chanya,” alisema Dk. Mwangi, akisisitiza mkakati wa benki ni wa mwaka 2030 unaozingatia Mpango wa Ufufuaji na Ustahimilivu wa Afrika (Africa Recovery and Resilience Plan – ARRP).

Aliongeza kuwa Equity inabadilika na kuwa “Taasisi ya Kifedha ya Mageuzi” inayojikita katika kukusanya mtaji na kuharakisha ustawi jumuishi na endelevu kote barani Afrika.

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button