“Erasto Nyoni alikuwa kasi”

LINDI: JESHI la Polisi Mkoa wa Lindi limebaini chanzo cha ajali ya basi la Timu ya Mpira wa Miguu ya Dodoma Jiji kutumbukia katika Mto Matandu ni kuwa dereva wa basi hilo Erasto Nyoni alikuwa kwenye mwendo kasi, pasipo kuchukua tahadhari ya ubovu wa barabara baada ya kuharibiwa na mvua msimu uliopita.

Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 12, 2015 na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Andrew Ngassa baada ya Kwenda kukagua eneo la tukio, ambapo amesema basi hilo lilikuwa linatokea Ruangwa na lilikuwa limebeba watu 36 miongoni mwao wachezaji walikuwa 24 pamoja na benchi la ufundi watu 12.

Soma zaidi: https://habarileo.co.tz/dodoma-fc-wapata-ajali-lindi/

Advertisement

“Gari hili lilikuwa linarudi Dodoma kupitia Dar es Salaam lilikuwa limebeba watu 36 miongoni mwao wachezaji walikuwa 24 pamoja na benchi la ufundi watu 12.

Lilipofika kwenye daraja la Matandu lilimshinda dereva na kutumbukia katika mto huo, na kusababisha majeruhi ya watu wanane,” amesema ACP Ngassa.

Soma zaidi: https://www.instagram.com/habarileo_tz/p/DF4zo3XC_te/

Ajali hiyo ilitokea Frbruari 10, 2025 majira ya saa tatu asubuhi katika Kijiji cha Matandu wilayani Kilwa wakati timu hiyo ilipokuwa ikisafiri kutoka wilayani Ruangwa kwenye mchezo wake na timu ya Namungo FC.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *