Fainali yabadili ratiba Ligi Kuu Bara

BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara imefanya mabadiliko ya tarehe ya michezo iliyosalia ya ligi hiyo.

Taarifa ya bodi hiyo imeeleza kuwa lengo la mabadiliko hayo ni kutoa nafasi kwa timu ya Yanga kucheza michezo yake miwili ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Algers ya Algeria itakayopigwa Mei 28, Dar es Salaam na ule wa mkondo wa pili utakaochezwa Juni 3, nchini Algeria.

Ligi kuu Tanzania Bara ilitarajiwa kumalizika Mei 28, lakini sasa michezo ya mwisho ya ligi hiyo itapigwa Juni 9, kwa timu zote kucheza siku moja, huku michezo ya  mzunguko wa 29 ikitarajiwa kupigwa Juni   6, ambapo bodi ya ligi imesisitiza kuwa lengo la kutoa nafasi hiyo ni kuhakikisha haki inakuwepo kwenye soka pamoja na kuepusha mazingira ya kupanga matokeo.

Habari Zifananazo

Back to top button