FCT yawajengea ujuzi wafanyabiashara Mwanza

MWANZA: Baraza la Ushindani (FCT) limetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara jijini Mwanza, yakilenga kuwaongezea uelewa kuhusu masuala ya ushindani wa soko pamoja na taratibu za kupata haki katika shughuli za kibiashara.
Katika mafunzo hayo yaliofanyika Febuari 5, wadau mbalimbali walijitokeza kuelezea walivyonufaika na mafunzo hayo na kusema wanapata ushirikiano mkubwa kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

Walisema serikali imeweka mazingira bora kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kupitia uwepo wa chombo huru cha kusimamia na kudhibiti ushindani wa soko ili kuleta usawa na kukuza uchumi wa taifa.
Akifungua semina hiyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana, amesema semina hiyo ni muhimu kwa wadau wa sekta ya biashara kwani itawawezesha kuelewa kwa kina majukumu ya Baraza la Ushindani pamoja na umuhimu wa mshikamano katika utekelezaji wa sheria za ushindani.

katika mafunzo hayo, Msajili wa Baraza la Ushindani, Mbegu Kaskasi, alisema Baraza lipo kwa ajili ya kulinda masuala yote yanayohusu ushindani wa soko na kuchochea maendeleo ya kiuchumi nchini. Alieleza kuwa kupitia utekelezaji wa majukumu yake, Baraza linaimarisha misingi ya utawala bora kwa kuhakikisha sheria za ushindani zinatekelezwa kikamilifu, kwa haki na kwa uwazi.
Aidha, aliongeza kuwa Baraza huhakikisha mamlaka za udhibiti zinazingatia taratibu na kanuni za ushindani wakati wa utekelezaji wa majukumu yao, sambamba na kutoa majawabu sahihi na ya haraka katika migogoro ya kibiashara.

Alibainisha kuwa hatua hiyo inalenga kumlinda mlaji dhidi ya vitendo vinavyodhoofisha ushindani, na hivyo kuchangia moja kwa moja katika ujenzi wa uchumi shindani, jumuishi na wenye tija kwa Watanzania.
Kwa upande wake, Hassan Karambi, Meneja wa Mkoa wa Chemba ya Wafanyabiashara, amesema amepata elimu yenye manufaa makubwa kupitia programu maalumu ya Baraza ya kuwajengea uwezo wadau.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yamewasaidia wafanyabiashara kutambua kuwa mdau au mfanyabiashara asiporidhika na maamuzi ya mamlaka za udhibiti kama LATRA, TCRA, TCAA, EWURA, PURA pamoja na Tume ya Ushindani (FCC), ana haki ya kukata rufaa katika Baraza la Ushindani ili kupata haki yake.
Naye Imelda Salumu, Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa, amefafanua utaratibu wa baraza katika kupokea rufaa kutoka kwa wadau.
Amesema kuwa malalamiko huanzia kwa mtoa huduma husika na endapo hayatapatiwa ufumbuzi, hufikishwa kwenye mamlaka ya udhibiti kama hatua ya kwanza ya rufaa.




I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com