FCT yatoa mafunzo kwa wadau Mbeya

MBEYA; Baraza la Ushindani (FCT) limefanya semina ya elimu kwa wadau kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu majukumu, mamlaka na huduma zinazotolewa na baraza hilo, pamoja na kuimarisha matumizi ya mifumo ya kisheria na kidijitali katika usimamizi wa rufaa.
Semina hiyo ilifunguliwa rasmi na Katibu Tawala Msaidizi – Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Mbeya, Anna Mwambene, ambaye aliwahimiza washiriki kutumia ipasavyo mifumo ya kisheria iliyopo katika kutafuta haki na kuwa mabalozi wa kuitangaza huduma za Baraza la Ushindani kwa wadau wengine.
Katika semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mbeya,, Baraza la Ushindani liliwapatia washiriki elimu kuhusu matumizi ya mfumo wa kidijitali wa kuwasilisha rufaa zinazotokana na maamuzi ya Tume ya Ushindani (FCC) pamoja na mamlaka za udhibiti zikiwemo LATRA, EWURA, TCRA, TCAA na PURA.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Ofisa wa TEAMA kutoka Baraza la Ushindani, Athuman Kanyegezi, ameeleza kuwa mfumo huo wa kidijitali unamwezesha mtumiaji kuanzisha akaunti, kuwasilisha rufaa kwa njia ya mtandao, kupakia nyaraka muhimu, kulipa ada husika na kufuatilia hatua za mwenendo wa kesi bila ulazima wa kufika ofisini, hivyo kuokoa muda na gharama.
Semina hiyo iliwahusisha wafanyabiashara, wajasiriamali pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za umma na binafsi, ambapo washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu taratibu za rufaa, matumizi ya mifumo ya kidijitali na upatikanaji wa haki kwa uwazi na ufanisi.




6.6 PROGRAMU ZA KIELELEZO
Mpango Elekezi 2050 umeainisha miradi 14 ya kielelezo. Miradi hii inalenga kuleta mageuzi ya viwanda nchini. Pia, itachochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi wa kijani. Itasaidia kukuza nguvukazi yenye ujuzi na maarifa ya kisasa. Aidha, miradi hii inalenga kuongeza ushindani wa Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa. Miradi hiyo imepangwa kama ifuatavyo:
NO PROGRAMME
1 Mageuzi ya Viwanda kwa Ukuaji wa Uchumi
2 Ujumuishaji wa Sekta ya Madini kwa Maendeleo ya Viwanda na Uchumi wa Kijani
3 Ubunifu wa Kidijitali na Miundombinu Mahiri kwa Ukuaji wa Siku za Usoni
4 Ujenzi wa Uhimilivu wa Tabianchi na Uchumi Endelevu wa Kijani
5 Kuendeleza Miundombinu na Muunganisho wa Usafiri kwa Tanzania kuwa Kitovu cha Kikanda
6 Mageuzi ya Sekta ya Nishati kwa Umeme Safi na Endelevu
7 Kukuza nguvukazi yenye Afya, Elimu na Ujuzi
8 Kuimarisha Utawala Bora, Uwajibikaji na Mifumo ya Udhibiti
9 Kuendeleza Miji Mahiri na Miundombinu Endelevu ya Mijini
10 Kuchochea Biashara, Uwekezaji na Upanuzi wa Uchumi
11 Kupanua Sekta ya Utalii na Uchumi wa Utamaduni
12 Kubadilisha Sekta ya Kilimo na Uchumi wa Vijijini
13 Kuboresha Elimu, Utafiti na Ubunifu wa Kiteknolojia
14 Mageuzi ya Kifedha ya Kidijitali na Jumuishi .