Fellain atundiga daruga

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Marouane Fellaini ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 36.
Mbelgiji huyo, ambaye alitumia misimu mitano na Everton, amemalizia maisha yake ya soka nchini China akiwa na Shandong Taishan.

Katika chapisho lake Instagram, Fellaini alisema: ‘Ninaandika chapisho hili kutangaza kwamba baada ya kazi ya miaka 18, ninastaafu soka la kulipwa.

‘Imekuwa safari ya ajabu. Nashukuru sana kucheza mchezo ninaoupenda kwa kiwango cha juu. Ninajivunia kuwakilisha Ubelgiji, Everton na Manchester United nchini Uingereza, na Shandong Taishan nchini China.” Ameandika Fellain.

Fellaini alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na David Moyes pale United kwa uhamisho wa pauni milioni 27.5 kutoka Everton siku ya mwisho mwaka 2013.

Akiwa United alishinda Kombe la FA. Kombe la Ligi na Ligi ya Europa katika miaka yake mitano na nusu Old Trafford, akifunga mabao 22 katika mechi 177.

Habari Zifananazo

Back to top button