Fidia mradi wa umeme yaanza kutolewa Karagwe

KARAGWE: WANANCHI 280 wa kata nne za wilaya ya Karagwe iliyopo mkoani Kagera wameanza kulipwa fidia na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) baada ya kupisha mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Benaco hadi Kyaka.

Wananchi hao walilazimika kupisha mradi huo kufuatia maagizo yaliyotolewa Mei 9, 2026 na Waziri wa Nishati, Deogratias Ndejembi.

Mhandisi aliyechora ramani na kupima ardhi kutoka Makao Makuu ya TANESCO, Derick Kaijanangoma, amesema jumla ya Sh bilioni 1.7 zimetolewa  kwa ajili ya ulipaji fidia katika awamu ya kwanza kwa wananchi wa kata za Nyaishozi, Nyakahanga, Bugene na Nyakasimbi

Amesema gharama za mradi za kulipa fidia ni Sh bilioni 6.1 na serikali imeanza kutoa fedha na wananchi wote wanaopisha ujenzi wa mradi huo ambao ni wilaya ya Ngara, Karagwe na Missenyi.

“Zoezi la ulipaji fidia tayari limefanyika katika wilaya ya Ngara na sasa linaendelea katika maeneo ya Karagwe tunajua kwamba tathmini ilifanyika mwaka 2022 lakini sasa muda wa kulipwa fidia umefika na kila familia itafikiwa hata kama muhusika amepoteza maisha kama anayoducumenti tumetoka vigezo atapatiwa haki yake, “alisema Kaijanangoma.

Alisema kuwa  kuwa baada ya kulipwa fidia, wananchi hawataruhusiwa kuendelea kufanya shughuli zozote za kibinadamu katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mradi, na wametakiwa kuondoa mali zao ndani ya siku 30, huku uwezekano wa kuongezewa muda ukiwepo pale inapobidi ili kumpa nafasi mkandarasi kuendelea na kazi.

Alitoa wito kwa Wananchi waliopokea fidia kuakikisha wanarudisha kilekile kiichofidiwa kama ni ardhi, nyumba, misitu na wasiitume pesa katika maswala mengine kama kuongeza mke au kukimbia familia.

Sarafina Gasiliel Ofisa Maendeleo ya Jamii wa mradi huo amesema changamoto kubwa ambazo wamekutana nazo katika ulipaji wa fidia ni migogoro ya ndoa , migogoro ya ardhi ambayo tayari imethaminishwa pamoja na ukosefu wa elimu ya mirathi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button