Fifa kuleta kadi ya bluu

IMERIPOTIWA Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) lipo katika mchakato wa majadiliano na waamuzi ya kuanzisha sheria ya uwepo wa kadi ya bluu.

Kwa mujibu wa mtandao wa OneFootball kadi hiyo itatumika kuonesha wachezaji wanapinga maamuzi ya waamuzi, kejeli na mengineyo.

Endapo mchezaji ataoneshwa kadi ya bluu, atatolewa uwanjani kwa dakika 10 nq baadaye kurejea tena.

Kwasasa kadi zinazotumika ni mbili, njano kuonya wachezaji wanapofanya madhambi, lugha chafu, au kupinga maamuzi na mengineyo, nyekundu kuondolewa uwanjani.

Habari Zifananazo

Back to top button