Funga mwaka Ligi Kuu wanawake

MICHEZO minne ya mzunguko wa tisa Ligi Kuu Wanawake (WPL) inapigwa leo viwanja tofauti.

Alliance Girls ya Mwanza itakuwa uwanja wa nyumbani wa CCM Kirumba kuikaribisha Simba Queens.

Mashujaa Queens ya Kigoma itakuwa ugenini kuivaa Bunda Queens kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma, Mara.

Nayo Ceasiaa Queens itakuwa mwenyeji wa Yanga Princess kwenye uwanja wa Somara mjini Iringa.

Funga mwaka nyingine itazikutanisha Mlandazi Queens na Fountain Gate Princess kwenye uwanja wa Kituo cha Ufundi cha TFF, Kigamboni Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Back to top button