ULAYA : MAWAZIRI wa mambo ya nje kutoka kundi la nchi saba tajiri duniani la G7 pamoja na nchi nyingine, wamelaani vikali kitengo cha Korea Kaskazini kupeleka wanajeshi wake Urusi.
Katika taarifa ya pamoja, wanadiplomasia hao wamesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutumika kwa wanajeshi hao katika uwanja wa vita nchini Ukraine.
Hatahivyo wamesema uungaji mkono wa Pyongyang katika vita hiyo Urusi dhidi ya Ukraine kutaongeza mzozo mkubwa utaoweza kuleta athari kubwa ya amani na usalama wa Ulaya na eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki.
SOMA: Ukraine yatawala mkutano wa G7 Italia
Taarifa hiyo ilitiwa saini na nchi za G7 pamoja na Australia, Korea Kusini, New Zealand na mjumbe mkuu wa Umoja wa Ulaya.