Gamondi alipochomoza katikati ya wazawa

NOVEMBA 4, mwaka 2025 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilimtangaza Miguel Gamondi kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, akichukua nafasi ya Mtanzania Hemed Suleiman ‘Morocco’.

TFF na Morocco walifikia makubaliano ya pande zote mbili kuvunja mkataba baina yao na sasa TFF chini ya Rais wake, Wallace Karia kuamua kuchukua muelekeo mwingine na kumtangaza Gamondi raia wa Argentina kuwa kocha wa muda wa Taifa Stars.

TFF imechukua muelekeo mwingine kwa sababu kupitia Karia, iliweka wazi dhamira yake ya kuwaamini makocha wazawa kuinoa Taifa Stars kwenye Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika Moshi, Kilimanjaro Desemba 21, mwaka 2024.

“Nitaendelea kuwaamini makocha wazawa,” alisema Karia kwenye mkutano huo wakati akimtambulisha Morocco sambamba na wasaidizi wake.

SOMA: Gamondi: Mbona freshi tu

Miezi 10 imepita tangu Karia atoe tamko hilo kwenye mkutano huo na sasa ameamua kuchukua muelekeo mpya, ikiwa ni mwezi mmoja umesalia kabla ya Taifa Stars haijaelekea nchini Morocco kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazoanza nchini humo Desemba mwaka huu.

Kwa kuchukua muelekeo mpya, ni sawa na kusema Karia ameamua kubadili mtazamo wake juu ya imani aliyoweka kwa makocha wazawa na sasa Taifa Stars itakuwa chini ya Gamondi anayetazamwa kuwa na uzoefu mkubwa wa soka la Afrika.

Kama bado angekuwa na imani na makocha wazawa, bado Karia alikuwa na machaguo mengi ya kuwapa jukumu hilo kuelekea michuano hiyo mikubwa kuliko yote kwa ngazi za timu za taifa kwa Afrika.

Kwenye orodha ambayo Karia angeweza kuwapa makocha wazawa jukumu hilo, wamo Charles Boniface Mkwasa, Abdallah Kibadeni, Salum Mayanga, Mecky Mexime, Adolf Rishard, Dk Mshindo Msolla na wengineo lakini ameamua kuweka matumaini yake makubwa kwa Gamondi ambaye kwa sasa anainoa Singida Black Stars.

Gamondi mwenye umri wa miaka 61 ana wasifu mkubwa na uzoefu wa soka la Afrika, akifundisha zaidi kwenye klabu mbalimbali na mara moja kuwa Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya taifa ya Burkina Faso.

Baadhi ya klabu alizowahi kuzifundisha ni pamoja na Wydad Casablanca, CR Belouizdad, Mamelodi Sundowns na Yanga, iliyomtambulisha na kumpa mafanikio zaidi katika soka la Tanzania kabla ya kuondoka na kurejea mwaka huu kuinoa Singida Black Stars.

Akiwa na Yanga, Gamondi alishinda mataji yote ya ndani sambamba na kuiwezesha timu hiyo kufika robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilipotolewa kwa mikwaju ya penalti na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini msimu wa mwaka 2023/2024.

Kwa namna yoyote ile, wasifu wake ni mkubwa pengine kuliko kocha yoyote mzawa na zaidi ya Morocco ambaye mafanikio yake makubwa ni kuiwezesha Taifa Stars kufuzu Afcon mwaka huu lakini kabla ya hapo hakuwa na wasifu mkubwa zaidi ya kuinoa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes na klabu mbalimbali za Ligi Kuu kama vile Geita, Namungo, Singida Black Stars, KMKM na klabu nyingine za Zanzibar.

Sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Congo na vipigo vya bao 1-0 kutoka kwa Niger na Zambia, Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar sio tu vilihitimisha ndoto ya Taifa Stars kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa na Canada, Marekani na Mexico mwakani lakini pia ziliibua mjadala miongoni mwa mashabiki wa soka wa Tanzania juu ya uwezo wa Morocco kuiletea mafanikio makubwa timu hiyo na pengine kupelekea Karia kuchukua muelekeo mpya na kuamua kurudi kwa makocha wa kigeni.

Akizungumzia uamuzi wa TFF kumpa Gamondi jukumu la kuinoa Taifa Stars, mchambuzi wa Azam Televisheni, Ramadhani Mbwaduke alisema ni uamuzi sahihi na ni kocha mwenye uzoefu mkubwa wa soka la Afrika. “Kwangu ni uamuzi sahihi, kwa sababu Gamondi ana miaka zaidi ya 20 Afrika tangu alipokuja mara ya kwanza mwaka 2000. Kwa wasifu huu, ni rahisi kuheshimika na wachezaji,” alisema Mbwaduke.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting websiteMore Details For Us→→ http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button