DAR ES SALAAM: MAKOCHA wa timu za Kariakoo, Yanga na Simba, Fadlu Davida na Miguel Gamond wameweka wazi namna watakavyoingia katika mchezo wa Derby yao utakaopigwa kesho uwanja wa Benjamini Mkapa jijini, Dar es Salaam.
Makocha hao wameweka mbinu zao walipozungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 18.
Kocha wa Simba,David ambaye ndiye mwenyeji wa mchezo huo amesema katika mechi ya kesho hawatoingia kwa kuzuia kama walivyofanya katika mechi zilizopita dhidi ya Yanga.
Kocha Fadlu kuelekea mchezo wa watani hapo kesho. #WenyeNchi #NguvuMoja pic.twitter.com/8SkaF50wCZ
— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) October 18, 2024
“Aina yetu mpira ni kushambulia huku tukiwa tumetawala mchezo, mechi iliyopita tulikuwa nyuma hivyo sio kila mechi tutaanza kukaba kutokea juu, kila mchezo una namna yake, timu yetu sio ya kukaa nyuma hatuna mchezo huo,”
Hata hivyo Kocha huyo amesema timu itakayokuwa na mbinu bora na mchezo mzuri Pamoja na wachezaji wake kujituma katika Derby hiyo ndiyo itakayoibuka na ushindi,” amesema.
Fadlu ameeleza kwamba anajua Derby itakuwa ngumu lakini wanaingia uwanjani kusaka alama sita wamejipanga kupata alama hizo katika michezo yao yote miwili.
Naye Kocha Mkuu wa Yanga, Gamond amesema, hana wasiwasi na wachezaji wake kuiendea dabi huku akifafanua kwamba watajitahisi kutofanya makosa kwa sababu wanaamini kosa moja linaweza kuwagharimu.
“Nani atavuna alama tatu muhimu, ninaamini wachezaji wangu watatekeleza hilo, mechi yetu dhidi ya Simba maandalizi hayana tofauri na mechi nyingine za Ligi Kuu,” amesema.
“Tunawaheshimu wapinzani wote tunaocheza nao ligi kuu. Ni kweli kesho tuna mechi ngumu kwani ni Derby, lakini tunajua namna tunauendea mchezo. Kila mara nasema mimi huwa sitazami sana historia. Yaliyopita yamepita, malengo yetu ni kutazama yanayokuja mbele yetu.” Miguel Gamondi… pic.twitter.com/mfW08zNa5S
— Young Africans SC (@YoungAfricansSC) October 18, 2024
Gamond amejinadi kwamba kutokana na ukubwa huo mashabiki na wapenzi wa soka wat imu hiyo wanatakiwa kuendelea kuisapoti timu yao na kuhusu idadi ya magoli watakayofunga itatokana na namna timu pinzani watakavyocheza.
Comments are closed.