Gamondi auwaza mziki wa Azam

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema licha ya kuwa na msimu mzuri bado wana kazi ngumu mbele yao katika fainali ya kombe la Shirikisho la CRBD dhidi ya Azam FC.

Kikosi cha Yanga kimeondoka leo kuelekea Visiwani Zanzibar na ajili ya fainali hiyo ya Juni 02, mwaka huu uwanja wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar, saa 2:15, usiku.

Gamondi amesema anafurahi kufikia malengo yao kwa kutwaa taji la ubingwa wa ligi pamoja na mchezaji wake Stephane Aziz Ki kufanikiwa kumaliza msimu akiwa kinara wa ufungaji.

“Licha ya yote lakini bado hatujamaliza kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni fainali, Azam FC wako vizuri tunatakiwa kuwa makini kuhakikisha tunafanikiwa kushinda mechi hiyo,” amesema Gamondi.

Amesema mchezo huo hautakuwa mchezo rahisi anaimani na vijana wake kufanya vizuri na kufanikiwa kutwaa taji hilo kama wakicheza vizuri na kufuata maelekezo yake.

“Msimu huu tumecheza vizuri, nimekuwa na timu bora, safu ya ulinzi, viungo na washambuliaji kisha kufanikiwa kuchukuwa tuzo ya ufungaji bora sasa tunaelekeza nguvu kwenye fainali yetu dhidi ya Azam FC.

Fainali ni timu mbili kati ya hizo lazima mmoja apate ushindi. Yanga kwangu ni timu bora kwa hapa nchini na tunaenda kucheza fainali kwenye uwanja mzuri ambao unachezeka vizuri,” amesema kocha huyo.

Gamondi ameeleza kuwa haitakuwa fainali rahisi kulingana na mechi ya mwisho walipokutana na Azam FC, walipoteza hali ambayo hataki kuona inajirudia katika fainali hiyo.

Habari Zifananazo

Back to top button