DODOMA: MTU mmoja (jina lake halijafahamika) amekufa katika ajili ya gari aina Toyota Alphard iliyotokea mkoani Dodoma, huku chanzo kikitajwa kuwa ni mwendokasi, na dereva kutokomea kusiko julikana.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) George Katabazi, ambapo amesema dereva wa gari hilo alijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari na kugongana na gari lingine kisha gari lake kupinduka na kusababisha kifo cha abiria mmoja aliyekuwamo katika gari hilo.
Soma zaidi: https://habarileo.co.tz/wapandishwa-vyeo-kuwa-wakaguzi-wasaidizi-wa-polisi/
Hata hivyo Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya ukaguzi na upekuzi na kukuta gari hilo likiwa na vifurushi sita vya dawa za kulevya aina ya mirungi vilivyo kuwa vikisafirishwa jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Aidha, Katabazi amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kumkamata dereva wa gari aliyekimbia pamoja na mmiliki halali wa gari hilo.
Soma zaidi: https://www.instagram.com/habarileo_tz/p/DF-ADaWug55/