GENEVA: SHIRIKA la ufadhili duniani Gavi limepanga kununua chanjo dozi 500,000 za Mpox kutoka kampuni ya Bavarian Nordic kwa ajili ya kusaidia kupambana na mripuko wa ugonjwa wa homa ya nyani barani Afrika.
Shirika hilo limepanga kutumia kiasi cha dola milioni 50 katika mpango huo, unaojumuisha usafirishaji, usambazaji na gharama za usimamizi wa chanjo.
Takribani dozi milioni 3.6 za Mpox tayari zimeahidiwa kutolewa na mataifa tajiri duniani kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lakini hadi sasa ni kiasi kidogo tu ambacho kimewasili.
SOMA : Afrika kunufaika na chanjo Mpox
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO mpaka sasa nchini DRC Congo kuna wagonjwa wa mpox 25,000 huku vifo 723 vilivyotokea katika Bara la Afrika.