Afrika kunufaika na chanjo Mpox

DENMARK : KAMPUNI ya Denmark ya kutengeneza dawa ya Bavarian Nordic imetia saini mkataba wa kusambaza dozi 440,000 ya chanjo dhidi ya homa ya nyani .

Afisa Mtendaji Mkuu wa  Kampuni hiyo Paul Chaplin amesema maombi ya kusambaza dozi hizo za chanjo yalijumuishwa kwenye makadirio yake ya mwaka huu.

Wiki iliyopita, kampuni hiyo ilisema iko tayari kutengeneza chanjo hadi dozi milioni 10 ya mpox ifikapo mwisho wa mwaka 2025.

Shirika la Afya  Duniani (WHO) imetoa wito wa kutengenezwa kwa chanjo huku kipaumbele kikiwa kwa nchi zilizoathirika zaidi na ugonjwa huo wa homa ya nyani.

SOMA: Tanzania kudhibiti Mpox

Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika, kimeeleza kuwa dozi 20,000 za chanjo zitasambazwa kote barani Afrika, kufuatia makubaliano kati ya Umoja wa Ulaya na kampuni ya kutengeneza dawa ya Bavarian Nordic.

 

Habari Zifananazo

Back to top button