Watoto 200 kupewa matibabu bure MOI

DAR ES SALAAM: Zaidi ya watoto 200 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi watapatiwa matibabu bure katika Taasisi ya Ubongo na Mishipa Muhimbili (MOI) mwaka huu .

Hatua hiyo imekuja mara baada ya MOI kusaini mkataba wa ushirikiano na Benki ya Azania ambayo wameahidi kutoa kiasi cha Sh milioni 200 kila mwaka kupitia mbio fupi za MOI Marathon zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa MOI, Balozi Dk Mpoki Ulisubisya amesema ushirikiano huo utaiwezesha benki hiyo kutoa kiasi hicho kugharamia matibabu ya watoto hao.

“Azania Benki imekuja wakati muafaka wakati tunaadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa MOI ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika na kuhitimishwa na mbio fupi za MOI marathon,” amesema Dk Mpoki.

Ameongeza kuwa makubaliano haya yatadumu kwa miaka mitatu na yatawezesha matibabu ya watoto ambao katika kila vizazi hai 1000 watoto Saba huzaliwa na tatizo hilo.

“Watoto wengi huja kwenye taasisi kama wakija fedha itakuwepo kwa ajili ya matibabu mchango huu utasaidia,Azania wanaunga mkono wachofanya Mo Dewji Foundation kusaidia watoto hao na watoto wanakuja katika nyakati tofauti.

Aidha, amewashauri akinamama watumie madini ya folic acid kabla ya mimba kwani ni muhimu inapungiza ukubwa wa tatizo na h wanapotumia dawa hizi wazitumie kwa umakini sana.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Azania Bank, Yahaya Mbanka amesema benki hiyo inajivunia kurudisha sehemu ya faida yake kwa kusaidia matibabu ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi kupitia MOI Marathon.

“Katika makubaliano haya Azania Benki inakwenda kutoka Sh milioni 200 Milioni kwa Taasisi ya MOI kupitia MOI marathon ili kuunga mkono jitihada za MOI kutoa matibabu kwa watoto hawa”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button