Gesi yajenga kituo cha afya na polisi

MTWARA: WANANCHI wa Msimbati, Wilaya ya Mtwara mkoani humo mbioni kunufaika na ujenzi wa kituo cha afya na kituo cha polisi katika eneo lao, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa serikali kurejesha katika jamii (CSR) inayozungukwa na mradi wa maendeleo.

Akielezea juu ya ujenzi huo Septemba 09 mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyolenga kukagua visima vya kuzalisha Gesi Asilia katika eneo la Mnazi Bay pamoja na miradi inayofanyika kwa manufaa ya jamii kutokana na uwepo wa gesi hiyo.

“Yote haya mnayoyaona ni matunda ya kazi nzuri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye anaonesha kwa vitendo jinsi anavyowajali kwa kuhakikikisha mnapata huduma bora kupitia miradi hii,” amesisitiza Kapinga

Ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ya Kamati ya Bunge ni kujionea  thamani ya miradi hiyo ambayo itanufaisha wananchi wa Msimbati, ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko aliyoyatoa Novemba 15, 2024 mara baada ya kutembelea eneo hilo na kuzungumza na wananchi.

Amesema ujenzi wa kituo cha Afya unatarajiwa kukamilika Septemba 30, 2024 huku ujenzi wa Kituo cha Polisi nao ukiwa ukingoni.

SOMA : Ruzuku kutolewa mitungi ya gesi 452,445

Kapinga amesisitiza kuwa, Serikali ipo pamoja na wananchi katika kuhakikisha inawapelekea maendeleo.

Katika hatua nyingine, Kapinga amewaasa wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa kwa kuanza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

SOMA :GESI MTWARA YAJENGA KITUO CHA AFYA, POLISI

Habari Zifananazo

Back to top button