WATU saba wamekufa baada ya lori lililobeba gesi kuwaka moto katika eneo Embakasi Nairobi nchini Kenya jana.
Taarifa ya Msemaji wa Serikali, Isaac Mwaura ilisema mchakato wa uchunguzi unaoendelea. Washukiwa wanne wa mlipuko huo walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkuu Milimani jana.
Washukiwa hao ambao kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Capitol Hill wanatarajiwa kufikishwa kortini kutoa uamuzi kuhusu ombi lao la kuzuiliwa.
Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilitaka kuwapata washukiwa; Derrick Kimathi (mmiliki wa kiwanda hicho), Joseph Makau, David Walunya Ong’are na Marrian Mutete Kioko waliwekwa rumande ili kukamilisha uchunguzi dhidi yao.
Wakati huo Linet Cheruiyot anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Embakasi. Anatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya Makadara.
Wakati huo huo, serikali iliongeza kuwa waathiriwa wote ambao walitafuta hifadhi katika Ukumbi wa Kijamii wa Embakasi wamejumuishwa katika orodha ya kupewa makazi mbadala.