RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itapunguza gharama za vyakula nchini.
Akizungumza leo wakati wa sala ya Ijumaa Msikiti wa Mubarak Bububu Kihinani, Mkoa wa Mjini Magharibi, Rais Mwinyi amesema atatoa namna ya kukabiliana na hali ya upandaji wa gharama za vyakula.
Rais Dk Mwinyi amesema atatoa taarifa muda mfupi ujao katika kukabiliana na hali ya upandaji wa gharama za vyakula ili kuwapunguzia mzigo wananchi.
Aidha amewahimiza waumini kutenda mema kwa kudumisha amani na kuwasaidia makundi ya wasiojiweza katika kuelekea kipindi cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan.