Gigy Money awachana wasanii

MSANII wa Bongofleva Gift Stanford, ‘Gigy Money‘ amesema kuwa wasanii wa bongo hawapendani wala hawasapotiani kwa jambo lolote.

Gigy Money amesema kuwa sio wote wanamoyo kama wake wa kusapoti na kuwapenda wengine ila wengi hawapendani.

“Mtu anaishi kama haitaji watu wengine kwenye maisha yao binafsi nawaitaji kiukweli tunategemeana ninachoona ni mtu kutotaka kuishi maisha yake, hatakikurudia nguo rudia tu ndo maisha yetu ya kibongo.

“amesema Gigy

Pia ameongeza kuwa “unakuta msanii anasema hana nguo ya kuvaa sio kweli vaa yoyote hata dera ni nguo ukitrendi umerudia nguo ila ni yako vaa tu binafsi ninawapenda na kusapoti ndo mana nina watu wanaonisapoti pia.”

Habari Zifananazo

Back to top button