Guinea: Aliyekuwa waziri wa ulinzi ahukumiwa miaka mitano jela

GUINEA: Mahakama nchini Guinea imemhukumu aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Mohamed Diane, kifungo cha miaka mitano jela kwa makosa ya rushwa, utajiri wa haramu, ubadhirifu na utakatishaji fedha.

Diane, ambaye alihudumu kama waziri wa ulinzi kati ya mwaka 2015 na 2021 chini ya Rais Alpha Condé, alikamatwa baada ya jeshi kupindua serikali.

Pia, ametakiwa kulipa faini ya dola za kimarekani milioni 58.5, huku akaunti zake za benki na mali zake ikiwemo nyumba zikitaifishwa. SOMA: Mamia wahofiwa kufa maporomoko New Guinea

Diane amekuwa kizuizini tangu Mei 2022, wakati utawala wa kijeshi ulipoanzisha kampeni kali dhidi ya ufisadi nchini Guinea.

 

Habari Zifananazo

Back to top button