Hakuna kiingilio Tamasha la Pasaka

Hakuna kiingilio Tamasha la Pasaka

TAMASHA la Pasaka linanatarajiwa kufanyika viwanja vya Leaders Club Aprili 9,2023 jijini Dar es Salaam na hakutakuwa na kiingilio.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Msama Promotion ambaye pia ni mwandaaji wa tamasha hilo,  Alex Msama amesema tamasha litakua la aina tofauti kwa kuwa waimbaji wote wataimba mubashara na hakuna kiingilio.

“Kuna wasanii wengi wakubwa wa muziki wa Injili kutoka nje watakuwepo, kuna ambao hawajawahi kufika Tanzania, ndio itakua mara ya kwanza kutumbuiza, “ amesema Msama.

Advertisement

Amesema kwa sasa wameanza kuweka mambo sawa kuhakikisha tamasha hilo pendwa linafanyika kwa ubora na kishindo kikubwa.

“Wapenzi na washabiki wa nyimbo za Injili wakae mkao wa kuzikosha nafsi zao, huku wakimtukuza Mungu kwa nyimbo za Injili.

”Tulikuwa kimya kwa muda mrefu kwa sababu mbalimbali, lakini kwa sasa tumeamua kurudi upya na tamasha letu pendwa la Pasaka, ” amesema Msama.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *