MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango amesema serikali inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda vya dawa, lakini kwa kuwa uamuzi huo ni wa Rais Dk. Samia Suluhi Hassan hakuna atakayefanikiwa kuvikwamisha, hivyo vitajengwa.
Amesema kwa sasa serikali inaagiza dawa kwa asilmia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90 kutoka nje ya nchi, hali inayosababisha uhaba wa vifaa na gharama kubwa za uagizaji wa vifaa vya afya hivyo ni lazima kuchukua maamuzi magumu.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda cha gloves kinachosimamiwa na Bohari ya Dawa ( MSD), Makamu wa Rais Dk. Mpango amesema serikali inatambua vita iliyopo katika ujenzi wa viwanda hivyo vya dawa.
Amesema Rais Dk. Samia ameamua viwanda hivyo vitajengwa kwa gharama yeyote kwa kuwa nchi ina uhaba wa dawa na vifaa tiba .
“ Bidhaa hizo zinaagizwa kutoka nje dawa zinaagizwa kwa asilimia 80 na vifaa tiba kwa asilimia 90 tumeamua kuipatia MSD majukumu manne ambayo ni uzalisha, ununuzi, utunzaji niwahakikishie viwanda hivi vitajengwa.
“Ujenzi wa viwanda hivi umelenga kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, kupunguza matumizi fedha za kigeni, uhaba wa dawa, gharama kubwa kuagiza bidhaa hizo na kutoa ajira,”amesema.
Amesifu hatua ya utekelezajiwa mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 90 kutoka asilimia 30 ambapo Rais Samia alikuta ujenzi ambao umekamilishwa na wataalamu wa ndani kwa kushirikisha Mamlaka husika.
Comments are closed.