‘Halmashauri Musoma Vijijini ichangie maabara masomo ya sayansi’

WANANCHI wa Musoma Vijijini wameiomba Halmashauri ya Wilaya hiyo (Musoma DC) ianze kuchangia ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayasi kwenye sekondari zake za Kata, tofauti na sasa ambapo inaratibu fedha zinazotolewa na serikali kuu.

Hayo yalielezwa jana na Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo, wakati akizungumzia uamuzi wa fedha zote za Mfuko wa Jimbo, kutumiwa kujengea Sekondari zote za Kata, Maabara za masomo ya Sayansi.

Jimbo hilo lenye Kata 21, lina Sekondari za Kata 25, kati ya hizoni Tatu tu zenye maabara za masomo ya Kemia, Baiolojia na Fizikia, nyingine zina maabara mbili, moja na nyingine hazina kabisa.

Kwa mujibu wa Profesa Muhongo, wameamua kujenga maabara hizo ili kila sekondari iwe na maabara tatu, huku ikiagizwa sekondari zinazojengwa na wananchi lazima ziwe na maabara hizo.

UJENZI wa Maabara Tatu za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia unaoendelea shuleni Mtiro, Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini.(Picha zote na Editha Majura).

“Mfano Sekondari ya Mtiro, Kata ya Bukumi yenye vijiji vya Buira, Bukumi, Buraga na Busekera iliyofunguliwa Mwaka 2006 haina maabara hata moja,” alisema Prof. Muhongo.

Alisema ina jumla ya wanafunzi 681 kati ya hao, 111 wanasoma Kidato cha Tatu 110 na wanalazimika kusoma somo la Baiolojia huku 14 wakisoma Fizikia na Kemia likisomwa na wanafunzi 17 tu.

Kidato cha nne alisema kina wafunzi 123, wote walazimika kusoma somo la Baiolojia, 21 wanasoma Fizikia na
26 Kemia hali aliyoielezea kuwa inaashiria mwitikio mdogo wa wanafunzi kwa masomo ya sayansi.

Alisema pia kuwa hiyo ni ishara ya umuhimu wa kuwepo Maabara za masomo hayo kwa ajili ya walinu kufundishia na wanafunzi kujifunzia kwa vitendo.

Licha ya fedha za mfuko wa jimbo, Sh Mil 1.508 zimechangwa kufuatia harambee iliyoitishwa na Mbunge huyo, kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa maabara tatu katika Sekondariya Mtiro.

Wakazi katika Kata ilipo shule hiyo wamechangia nguvu kazi katika kuchimba misingi, kusomba mchanga roli 27, kokoto roli mbili na saruji mifuko nane.

Mbunge huyo aliahidi kuchangia mifuko 200 ya saruji na nondo 49, alitoa mifuko 75 huku akitoa wito kwa wazaliwa wa Musoma Vijijini waanze au waendelee kuchangia ujenzi huo.

Habari Zifananazo

Back to top button