Hamas yakataa mpango wa Trump

GAZA,PALESTINA : KUNDI la Wanamgambo la Hamas limesema liko tayari kusitisha mapigano na Israel, lakini haiko tayari kuunga mkono mpango uliotangazwa na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Hamas imesisitiza kuwa makubaliano yoyote ya kweli ni lazima yajumuishe kusitishwa kikamilifu kwa vita katika Ukanda wa Gaza, ikiwa ni msimamo wao wa muda mrefu.

Rais Trump alitangaza kuwa Israel imekubali kusitisha mashambulizi kwa siku 60, na kuitaka Hamas kuridhia mpango huo kabla hali haijazidi kuwa mbaya.

Hata hivyo, Israel imesisitiza kuwa haitaafiki mpango wowote wa kudumu hadi itakapofanikiwa kulisambaratisha kabisa kundi la Hamas. SOMA: Jeshi la Israel lashambulia Gaza

Trump ameendelea kutoa shinikizo kwa pande hizo mbili kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano, kuwaachia mateka wanaoshikiliwa na Hamas na kusitisha kabisa vita vilivyodumu kwa takribani miaka miwili.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button