Jeshi la Israel lashambulia Gaza

ISRAEL : JESHI la Israel limefanya mashambulizi ya anga katikati na kusini mwa Gaza, likilenga wanamgambo waliokuwa wakijaribu kutega mabomu karibu na vikosi vyake katika ukanda huo.

Mamlaka za Palestina zimetangaza kuwa watu watatu wameuawa katika mashambulizi hayo.

Jumamosi, Israel ilifanya mashambulizi mengine kwenye mji wa Beit Lahia kaskazini mwa Gaza, ambapo watu tisa, wakiwemo waandishi wa habari wanne wa Kipalestina, waliuawa.

Advertisement

Kundi la Hamas limeukana mashambulizi hayo, likisema kuwa ni ukiukaji mkubwa wa makubaliano ya usitishaji mapigano. SOMA: Israel yasitisha huduma ya umeme Gaza

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *