Hapa ndipo alipozikwa Papa Francis

ROME : KABURI la Papa Francis limeanza kuonyeshwa kwa umma katika kanisa la Santa Maria Maggiore mjini Rome.
Papa Francis alizikwa siku ya jumamosi katika kanisa hilo ikiwa ni mojawapo ya makanisa makubwa manne ambayo aliyapendelea kuyatembelea katika mji mkuu wa Italia.

Maelfu ya waombolezaji wamekuwa wakitembelea kaburi lake tangu kanisa hilo kufunguliwa kwa umma Jumapili asubuhi ili kutoa heshima zao kwa Papa Francis, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 88 siku ya Jumatatu ya Pasaka.



