Harmonize hafaidiki na nyimbo zake
Msanii Rajab Abdul ‘Harmonize’ amedai hajawahi kupata fedha kutokana na usambazaji wa nyimbo zake kwenye mitandao kwa kipindi cha miaka saba.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram (Instastory) msanii huyo ameeleza kuwa anapopoleka miziki yake kwa wasambazaji kuna kampuni ambayo inajitambulisha kuwa ndio wamiliki wa kazi hizo.
“Ni muda wa kukomesha hili msitumie udhaifu wa watu kujinufaisha, kumbuka napaswa kuongelea hili kwa ajili ya watu wengine.” Amendika Harmonize.
Harmonize ameeleza kuwa kwa sasa anatafuta kampuni ya usambazaji na wachapishaji wa muziki wake ili kuepuka sintofahamu anayoipitia.