Hatua zaanza ujenzi bandari Mtwara

SERIKALI ipo mbioni kuanza ujenzi wa bandari nyingine katika mkoani Mtwara katika eneo la Kisiwa Mgao ambapo kwa sasa hatua za manunuzi zimeanza.

Akizungumza na mkoani Mtwara wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa bandari ya Mtwara Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema, bandari hiyo mpya itakuwa ni maalumu kwa ajili ya usafirishaji bidhaa zijulikanazo kama ‘bidhaa chafu’ ambazo ni k makaa ya mawe na saruji.

Amesema Wizara ya Uchukuzi inaendelea kuweka mikakati ya namna ya kuimarisha Bandari ya Mtwara ili kuhakikisha bidhaa nyingine pia zinasafirishwa kwa wingi.

Aidha, Kihenzile pia, ametembelea na kukagua utendaji kazi wa bandari ya Mtwara na uwanja wa ndege wa Mtwara.

Habari Zifananazo

Back to top button