Haya hapa matokeo kidato cha sita

BARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023.

Akitangaza matokeo hayo leo Julai 12, 2023 katika ofisi za Baraza hilo Zanzibar, Katibu Mtendaji wa Necta Dk Said Mohamed amesema jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani ni 106, 883 huku wasichana wakiwa ni 47, 340 na wavulana 59, 543.

“Jumla ya watahiniwa 104,549 sawa na asilimia 99.23 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita 2023 wamefaulu.” amesema.

Advertisement

Wasichana waliofaulu ni 46,707 sawa na asilimia 99.51 huku kwa upande wa wavulana, waliofaulu ni 57, 843 sawa na asilimia 99.

MATOKEO BONYEZA HAPA>>>>> https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/dsee/index.htm

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *