Hekaheka EPL, Serie A, Ligue 1 leo
IKIWA ni siku ya nne ya mwaka mpya 2025, michezo ya Ligi Kuu England(EPL), Italia(Serie A) na Ufaransa(Ligue 1) inaendelea leo kwenye viwanja kadhaa.
Liverpool inaongoza msimamo EPL ikiwa na pointi 45 baada ya michezo 18 huku Southampton ikishika nafasi ya 20 mwisho wa msimamo ikiwa na pointi sita.
Katika Serie A, Atalanta ni vinara ikiwa na pointi 41 baada ya michezo 18 wakati Monza ni mwisho katika msimamo ikiwa na pointi 10.
Bingwa mtetezi Ligi Kuu Ufaransa, Paris Saint-Germain inaongoza Ligue 1 ikiwa na pointi 40 baada ya michezo 18 huku Montpellier inayoshika nafasi ya 18 mwisho wa msimamo ina pointi tisa.
Mitanange inayopigwa leo ni kama ifuatavyo:
PREMIER LEAGUE
Tottenham Hotspur vs Newcastle United
Aston Villa vs Leicester City
Bournemouth vs Everton
Crystal Palace vs Chelsea
Manchester City vs West Ham United
Southampton vs Brentford
Brighton vs Arsenal
SERIE A
Venezia vs Empoli
Fiorentina vs Napoli
Hellas Verona vs Udinese
LIGUE 1
Saint-Etienne vs Reims
Lille vs Nantes
Lyon vs Montpellier



