Hezbollah yatangaza ushindi

LEBANON : KUNDI la Hezbollah limetangaza ushindi dhidi ya Israel baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, likisema wapiganaji wake wako tayari kukabiliana na vitisho vya Israel siku zijazo.

Licha ya vikosi vya Israel kusababisha hasara kubwa kwa kundi hilo ikiwemo kuuawa kwa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah lakini Israel ilishindwa kuchukua miji yoyote kadhalika na kutenga eneo lao la kiusalama .

Mkataba huo wa kusitisha mapigano unaitaka Hezbollah kuondoka kaskazini mwa Mto Litani na kuvunja miundombinu yake ya kijeshi kusini mwa Lebanon.

Advertisement

Hatahivyo, Hezbollah ilidai ilifanya zaidi ya operesheni 4,637 za kijeshi dhidi ya Israel tangu Oktoba 2023 na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono Wapalestina.

SOMA: Israel kujadili azimio la Beirut