Israel kujadili azimio la Beirut

LEBANON: SERIKALI ya Israeli iko tayari kupitisha mpango wa Marekani wa kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah.

Hivi sasa Baraza la Usalama la Israel linatarajia kukutana baadaye leo Jumanne ili kujadili na kuidhinisha mpango huo katika kikao maalum kitakachoongzowa na  Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Tayari mkataba huo umeshaidhinishwa mjini Beirut, ambako Naibu Spika wa Bunge la Lebanon, Elias Bou Saab ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa hapakuwa na vikwazo vyovyote vitakavyozuia makubaliano hayo yashindwe kutekelezwa.

Advertisement

Bou Saab  ameongezea kuwa mpango huo utawataka wanajeshi wa Israel kuondoka kusini mwa Lebanon kadhalika na wanajeshi wa Lebanon watahitajika kurejea  katika ngome ya Hezbollah iliyokuwepo maeneo ya mpakani ndani ya siku 60.

Soma: Hezbollah kulipiza mashambulizi