LEBANON : HEZBOLLAH imetangaza kurusha makombora katika kambi ya jeshi la wanamaji la Israel na uwanja wa ndege wa kijeshi karibu na mji wa Haifa kwa mara ya pili katika muda wa chini ya saa 24, huku kukiwa na makabiliano ya wazi kati ya pande hizo mbili.
Kundi hilo limesema wapiganaji wake wamelenga kuishambulia kambi ya wanamaji ya Stella Maris, iliyoko kaskazini-magharibi mwa Haifa.
Pia wamepanga kulenga kambi nyingine ya Ramat David na uwanja wa ndege, kusini mashariki mwa Haifa kwa msururu wa makombora na yenye ubora.
Uamuzi huu umekuja kujibu mashambulizi hayo mawili yamekuja kujibu mashambulizi na mauaji yaliyofanywa na Israel nchini Lebanon.