BEIRUT : ISRAEL imefanya mashambulizi mengine manne ya anga katika eneo la kusini mwa mji wa Beirut baada ya jeshi hilo kuwahimiza watu waondoke katika ngome ya Hezbollah .
Kwa mujibu wa Shirika la habari nchini humo -NNA limeripoti kutokea kwa mashambulizi hayo ambayo yalitokea katika maeneo tofauti ikiwemo maeneo ya kusini katika eneo la Saint Therese na mashambulizi mengine yakipigwa huko Burj al-Barajneh.
SOMA : Jeshi la Israel laingia Lebanon
Hatahivyo, Kikosi cha Kijeshi cha Israel -IDF kimekiri kufanya mashambulizi hayo katika ngome za Hezbollah ikiwemo maghala ya silaha mjini Beirut.