Wanajeshi nane israel wauawa

LEBANON : JESHI la Israel limethibitisha wanajeshi wake wanane wameuawa kwenye mapigano yanayoendelea dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah, kusini mwa Lebanon, siku moja baada ya kuanza kile kilochotajwa kuwa operesheni maalum ya ardhini inayolenga kuharibu miundombinu ya kundi hilo.

“Tupo kwenye vita vikali dhidi ya kundi la Iran linalopanga kutuangamiza,” alisema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

“Hilo halitawezekana kuwa tutasimama pamoja na kushinda, Mungu akiwa nasi,” aliongeza kusema.

Advertisement

Jeshi la wanahewa la Israel lilifanya mashambulizi ya anga usiku kucha kwenye ngome za Hezbollah, kusini mwa mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

Mwanzoni mwa wiki hii, wizara ya afya ya Lebanon ilisema kuwa takriban watu 55 waliuawa na wengine 156 kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya Israel ndani ya saa 24 zilizopita.

Hali ya tahadhari inazidi kuongezeka  kufuatia mashambulizi ya makombora takriban 200 yaliyorushwa na Iran ndani ya Israel.

Iran ilifanya mashambulizi hayo wakati wa mkesha wa Siku Kuu ya Mwaka Mpya ya Wayahudi, yakiwa ya kulipiza kisasi cha mashambulizi kutoka Israel , yaliouwa viongozi kadhaa wa kipalestina ndani ya Labanon.

 SOMA:  UN, Lebanon waomba ufadhili dola mil 426