UN, Lebanon waomba ufadhili dola mil 426

GENEVA : MSEMAJI wa kuratibu shughuli za wakimbizi  UN, OCHA, Jens Laerke amewaambia waandishi wa habari kuwa Umoja wa Mataifa na Serikali ya Lebanon imeomba ufadhili wa dola milioni 426, ili kutoa misaada ya dharura ya kibinadamu kwa watu milioni moja walioathiriwa na mzozo unaoendelea nchini humo.

“Ndani ya wiki mbili zilizopita, zaidi ya watu 1,000 wameuwawa huku wengine zaidi ya 6,000 wakijeruhiwa na wengine milioni kuathirika moja kwa moja au kukoseshwa makazi tangu Okotoba 2023, “amesema Jens Laerke.

, “Ningependa kuongeza kusema kuwa saa chache zilizopita, tumepata ripoti za kuanza kwa mashambulizi ya ardhini kutoka Israel kusini mwa Labanon,” amesema Laerke.

Amesema kuwa tayari UN pamoja na mashirika yasio ya kiserikali wameanza kutoa misaada ya chakula , na lishe bora kwa watoto, maji pamoja na misaada mingine ya msingi kwa waathirika.

SOMAIsrael yashambulia Lebanon

Israel imesema kuwa mashambulizi yake yataendelea hadi pale Hezbollah itakapositisha kurusha roketi ndani ya Israel, na pale ambapo hali itakuwa salama kwa familia zinazoishi karibu na mpaka wa Lebanon.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button