Israel yashambulia Lebanon

LEBANON : ISRAEL imewashambulia wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon masaa machache baada ya kiongozi wao, Hassan Nasrallah, kuapa kulipiza kisasi mashambulizi ya kieletroniki yaliyouwa watu 37 na kuwajeruhi maelfu ya wengine.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon Abdallah Bou Habib amesema shambulio hilo ni la wazi dhidi ya mamlaka na usalama wa Lebanon na kwamba linahatarisha eneo zima kutumbukia katika vita.

“Shambulio lolote litakalozidisha hali ya mvutano katika eneo hilo halitasaidia kupunguza mvutano huo. Hakika tunachotaka ni kuona makubaliano ya kusitisha mapigano yanafikiwa. Tunataka kuona mateka wakirejea nyumbani. Tunataka kushuhudia vita vya Gaza vikimalizika.” Alisema naibu katibu wa masuala ya habari katika wizara ya ulinzi ya Marekani, Sabrina Singh.

Hata hivyo, maafisa kadhaa wa Marekani wamesema wanaamini kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas huko Gaza hayawezekani kabla ya Rais Joe Biden kuondoka madarakani mwezi Januari.

SOMA :  Qatar yatarajia mapatano zaidi Israel, Hamas

 

Habari Zifananazo

Back to top button