Jeshi la Israel laingia Lebanon

Wanajeshi wa ardhini wa Israel wamevuka mpaka kuingia kusini mwa Lebanon mapema leo kuwakabili wapiganaji wa kundi la Hezbollah.

Hatua hiyo inafuatia wiki kadhaa za mashambulio ya anga ya Israel dhidi ya Hezbollah likiwemo shambulizi  lililomuua kiongozi wa muda mrefu wa kundi hilo Hassan Nasrallah, kundi ambalo lilianza kurusha makombora kuelekea Kaskazini mwa Israel baada ya vita ya Gaza kuanza.

SOMA: Jeshi la Israel: Hassan Nasrallah amekufa

Mara ya mwisho Israel and Hezbollah kupigana vita ya ardhini ilikuwa 2006 iliyodumu mwezi mmoja.

Taarifa fupi ya jeshi la Israel imesema jeshi hilo limeanza mashambulizi ya ardhini yenye mipaka, eneo maalum na yenye malengo dhidi ya Hezbollah Kusini mwa Lebanon.

“Maeneo yanayolengwa ni vijiji karibu na mpaka na ameneo haya yanahatarisha usalama kwa jamii za waisrael Kaskazini mwa Israel,” imesema taarifa hiyo.

Hakuna maelezo oparesheni hiyo itadumu kwa muda gani.

Israel imesema itaendelea kushambulia kundi hilo hadi kumekuwa na usalama kwa waisrael waliohama makazi mpakani kurejea kwenye nyumba zao.

 

Habari Zifananazo

Back to top button