Jeshi la Israel: Hassan Nasrallah amekufa

Kiongozi wa kundi Hezbollah, Hassan Nasrallah.

JESHI la Israel leo limetangaza ramsi kumuua kiongozi wa kundi Hezbollah, Hassan Nasrallah, siku moja baada ya kufanya shambulio kubwa la anga Lebabon.

“Hassan Nasrallah amekufa,” Msemaji wa Jeshi la Israel Luteni Kanali Nadav Shoshani amesema kupitia mtandao wa kijamii wa X.

Advertisement

Jeshi Ulinzi la Israel(IDF) limesema Nasrallah ameuawa Septemba 27 wakati ndege za kivita zilipokamilisha kile lilichokiita “shambulio lengwa” katika makao makuu ya Hezbollah yaliyopo mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

SOMA: Israel yashambulia Lebanon

IDF imesema miongoni mwa makamanda wengine wa Hezbollah, kamanda wa mstari wa mbele Kusini Ali Karki, pia ameuawa katika shambulio hilo

Hakuna kauli au taarifa zilizolewa na Hezbollah.

Nasrallah ameongoza hezbollah inayoungwa na mkono na Iran kwa zaidi miongo mitatu.