NIDA kuanza kusajili watoto

DODOMA; MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inatarajia kuanza kufanya usajili wa watoto kuanzia umri wa kuzaliwa, ili kutoa namba ya utambulisho ya kipekee ambayo itajulikana kama Jamii Namba.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 25, 2026 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2026/27.

“Katika mwaka wa fedha 2026/27, Wizara kupitia NIDA itaendelea kusajili na kutambua watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea na kuwapatia Vitambulisho vya Taifa.

“Aidha, NIDA inatarajia kuanza kufanya usajili wa watoto kuanzia umri wa kuzaliwa ili kutoa namba ya utambulisho ya kipekee ambayo itajulikana kama Jamii Namba.

“Namba hiyo itatumika katika kupatiwa huduma mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kiusalama tangu mtu anapozaliwa hadi mwisho wa maisha yake,” amesema Waziri Katambi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button