Hili pia tumelikosa dah!

MANYARA; HILI tunabeba! Ilikuwa kaulimbiu ya Simba kuelekea mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho la Afrika dhidi ya RS Berkane uliofanyika Mei 25, 2025 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Lakini mambo hayakwenda kama ilivyotarajiwa, Simba ikatoka sare ya bao 1-1, ikaachia kombe likienda Morocco kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza ambao Simba ilifungwa mabao 2-0 nchini Morocco, hivyo kwa kulikosa Kombe la Shirikisho Afrika ikatamka kuwa inahamishia nguvu kwenye Ligi Kuu ya NBC na michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB.

Leo Simba ikajitupa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mkoani Manyara ikiivaa Singida Black Stars, ambayo Jumatano wiki hii ilifungwa bao 1-0 na Simba Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.

Lakini mashabiki wa Simba walijikuta baada ya dakika 90 za mchezo huo kwenye makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii wanasema: “Hili pia tumelikosa.” Kauli ambayo pia inatumiwa kuwatania kutoka kwa mashabiki mbalimbali wa mpira. Kwa nini wamelikosa?

Ni kutokana na kipigo cha mabao 1-3, ambacho Simba imekipata kutoka kwa Singida Black Stars na hivyo kuzima ndoto za kutinga fainali na kunyakua kombe hilo kama walivyokuwa wamepanga. Singida sasa itacheza fainali na Yanga, ikiwaacha Simba wakiwa na huzuni na maneno ya mashabiki ni: Hili pia tumelikosa!

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button