Huduma afya ya akili kuboreshwa

DODOMA : NAIBU WAZIRI wa Afya, Dk. Godwin Mollel amesema serikali imepanga kuboresha utoaji wa huduma za afya ya akili na utengamano katika hospitali za mikoa nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza ustawi wa afya ya akili kwa wananchi.
Akijibu swali bungeni jijini Dodoma, Dk. Mollel amesema serikali imekuwa ikiendelea kuboresha huduma hizo kwa kuzingatia mahitaji ya kisasa ya tiba kwa wagonjwa wa afya ya akili.
“Serikali inalenga kuweka huduma za kisasa katika hospitali zetu ili kuhakikisha kuwa wagonjwa wa afya ya akili wanapata matibabu bora na ya kisasa,” amesema Dk. Mollel.