Ibada Ijumaa Kuu, Pasaka kufanyika Ruvuma

JUMUIYA ya Kikristo Tanzania (CCT) imesema ibada za Ijumaa Kuu na Sikukuu ya Pasaka kitaifa mwaka huu zitafanyika Mkoa wa Ruvuma.

Ofisa Habari wa CCT, Mchungaji John Kamoyo alisema Ibada ya Ijumaa Kuu ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha Yesu Kristo itafanyika katika Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi (KIUMA) lililopo mkoani Ruvuma.

Pia alieleza kuwa Misa Takatifu kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka, inayoadhimishwa kukumbuka Ufufuko wa Yesu Kristo, itafanyika kitaifa katika Kanisa Katoliki Ruvuma.

Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padre Chesco  Msaga alisema Misa Takatifu ya Pasaka itaanza saa moja na nusu asubuhi katika Parokia ya Mtakatifu Fransisco Ekisaveri, Kanisa Kuu Jimbo Katoliki Tunduru Masasi.

Alisema misa hiyo itaendeshwa na Askofu wa Jimbo Kuu la Tunduru Masasi, Filbert Mhasi na kuoneshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha TBC.

Akizungumzia sikukuu hizo, Mchungaji Kamoyo aliwataka Wakristo kukumbuka maadhimisho hayo ya kifo na ufufuko wa bwana Yesu Kristo kwa kuwa na upendo wa dhati kwa wahitaji na watu wenye shida mbalimbali.

Habari Zifananazo

Back to top button