Ibrahim Bacca afungiwa mechi 5

DAR ES SALAM; BEKI wa Yanga ya Dar es Salaam, Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ amefungiwa michezo mitano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi Ibrahim Ame wa Mbeya City, wakati wa mchezo baina ya timu hizo Jumanne wiki hii mkoani Mbeya.
Uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kilichofanyika jana Oktoba 2, 2025.



