Ibungiro yatinga nusu fainali Angeline Jimbo Cup

KATA ya Ibungiro imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga kata ya Ilemela bao 1-0 katika mchezo wa robo fainali wa mashindano ya Angeline Jimbo 2023 uliochezwa leo katika uwanja wa shule ya msingi ya Sabasaba wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Moses Peter katika dakika ya 13.Mchezo mwingine utakaochezwa kesho itakuwa kati ya kata ya Sangabuye dhidi ya Nyakato.

Septemba 6 kata ya Kirumba itacheza dhidi ya Nyasaka huku mchezo wa mwisho wa robo fainali utachezwa Septemba 7 kati ya Shibula itacheza dhidi ya Mecco.

Naye katibu wa mbunge wa jimbo la Ilemela, Charles David amewaomba wakazi wa manisapaa ya Ilemela wajitokeze kwa wingi katika michezo ya robo fainali inayoendelea katika uwanja wa shule ya msingi Saba.

Katibu mkuu wa chama cha soka Wilaya ya Ilemela (IDFA) Almas Moshi amesema timu zitakazofuzu hatua ya nusu fainali zitapewa jezi.

Habari Zifananazo

9 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button