ICJ yaanza kusikiliza kesi ya mabadiliko tabianchi

UHOLANZI : MAHAKAMA ya Juu ya Umoja wa Mataifa mjini The Hague, inasikiliza kesi kubwa kabisa ya kihistoria kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.
Mataifa madogo ya visiwa yamepeleka vilio vyao mbele ya mahakama hiyo ya kimataifa ya haki – ICJ kuhusiana na athari kubwa za mabadiliko ya tabia nchi wanazohisi zinatishia uhai wa visiwa vyao.
Pia wametaka mataifa makubwa yanayochafua mazingira yabebeshwe jukumu hilo la kutatua tatizo la mabadiliko ya tabianchi.
Mwaka jana Baraza kuu la Umoja wa Mataifa liliomba mahakama hiyo ya kusuluhisha migogoro ya Kimataifa, kutowa msimamo wake kuhusu wajibu wa mataifa makubwa kuhusu suala la mabadiliko ya tabia nchi. SOMA:Mikakati yawekwa kukabili mabadiliko ya tabia nchi
Hatua hiyo ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa ilikuja kufuatia miaka kadhaa, ya mataifa ya visiwa yalikuwa na hofu ya kutoweka kwa visiwa vyao na kulishawishi baraza hilo kutafuta suluhisho la kudumu.



