Idadi ya wagonjwa saratani kuongezeka duniani

RIPOTI mpya iliyochapishwa na jarida la masuala ya tiba la Lancet inaonyesha idadi ya wagonjwa wapya wa saratani itakua kwa kasi duniani. Wagonjwa wanatarajiwa kuongezeka kutoka milioni 18.5 mwaka 2023 hadi milioni 30.5 mwaka 2050.
Watafiti wa masuala ya afya wanasema ongezeko hili linatokana na jamii kuwa na idadi kubwa ya wazee ambao ni wahanga wakubwa wa saratani. Pia, idadi ya vifo kutokana na saratani inatarajiwa kufikia milioni 10.4, sawa na asilimia 42 ya vifo vyote vilivyotokea mwaka 2023.
Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa sababu kubwa za ongezeko la wagonjwa ni matumizi ya tumbaku, ambayo yamesababisha asilimia 21.4 ya vifo vya saratani, hasa katika nchi masikini na zinazoendelea. Ngono isiyo salama pia imesababisha maambukizi ya virusi vya HPV, vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi.
Ripoti hii ya ongezeko la wagonjwa wa saratani na visababishi vya saratani imehusisha nchi zisizopungua 204 duniani, ikitoa taswira ya kina ya mzigo wa saratani duniani kote. SOMA: Ukaguzi wa mate wapendekezwa kubaini saratani ya tezi dume