Idd kitaifa Dar, Samia mgeni kwenye Baraza
DAR ES SALAAM: SHEREHE za Sikukuu ya Eid el-Fitri zinatarajiwa kuwa Machi 20 au 21. 2026 kutegemea mwandamo wa mwezi.
Taarifa iliyotolewa leo Machi 12, 2026 na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Alhaji Nuhu Mruma imesema swala ya Idd kitaifa itaswaliwa Msikiti wa Mfalme Mohamed VI, Kinondoni, Dar es Salaam.
“Swala ya Eid itaswaliwa Msikiti wa Mfalme Mohamed VI uliopo Makao Makuu ya BAKWATA Kinondoni kuanzia saa 1:30 asubuhi, huku Baraza la Eid likifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa 9:00 mchana,” imefafanua taarifa hiyo na kuongeza kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Idd anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.




Vyombo vya habari vinapaswa kufuata matamko ya viongozi wa kidin mfano pale muft wa tanzania alpotangaza kuwa eid el fitr itakuwa machi,2026 vyombo vya habari kama TV IMAAN TANZANIA visingeendelea kuchanganya watu juu ya suala la sikukuu ya eid.